
Samuella H.
Lowell High School
Class of 2021
KUHUSU CHUO KIKUU CHA MAPEMA CHA LOWELL
Chuo kikuu cha mapema cha lowell ni fursa bora zaidi ya kimasomo iliyofunguliwa kwa wanafunzi wote wa shule ya upili ya Lowell High School students bila kujali ni nini wanaopanga kufanya baada ya kuhitimu
Programu hiyo huwakubali wanafunzi wapate masomo ya kuwanufaisha ya kiwango cha chuo kikuu ilihali bado wamo katika shule ya upili, kupata alama za kiukweli za chuo kikuu, na kufanya mwanzo wa mapema kwa maisha yao ya baada ya shule ya upili na kazi—bila gharama yoyote kwao au kwa familia zao.
NAMNA INAVYOFANYA KAZI
Anza Elimu Yako ya Chuo Kikuu SASA!
Masomo ya chuo kikuu cha mapema huwapatia wanafunzi wa shule ya upili mwanzo wa mapema kwa kwa masomo yao ya chuo kikuu huku wakijenga matamanio, ujuzi, na kujiamini itakayowasaidia kufanikiwa baada ya kuhitimu shule.
Chukua Masomo Bure ya Chuo Kikuu
Masomo ya chuo kikuu cha mapema ni bure kwa wanafunzi wanaohudhuria Lowell High School—gharama hulipiwa kupitia ufadhili wa eneo, programu za jimbo, na misaada ya kibinafsi.
Pata Alama za Shule ya Upili na Chuo Kikuu
Wanafunzi wa chuo kikuu cha mapema hupata alama za masomo kutoka Lowell High School na Middlesex Community College pia—yaani, wanafunzi hupata alama za masomo mara mbili kwa kila somo wanaokamilisha na mafanikio.
Kuhamisha Alama Baada ya Kuhitimu
Alama za chuo kikuu cha mapema ni alama za uhakika za chuo kikuu na zinaweza kuhamishwa kwa vyuo vikuu kote Marekani.
Pokea Utegemezi wa Moja kwa Moja
Wanafunzi wote wa chuo kikuu cha mapema na familia zao hupokea ushauri wa kibinafsi na uongozi wa mfano—timu yetu ya utegemezi itawaongoza katika kila hatua ya mchakato huu.
Shiriki Katika Mashughuli Nje ya Mtaala
Wanafunzi wa chuo kikuu cha mapema huweza kuchukua masomo kutoka chuo cha Middlesex Community College cha mjini, bali pia huweza kushiriki katika programu na mashughuli katika chuo kikuu kama tu wanafunzi wa muda kamili wa chuo kikuu.
TAARIFA MUHIMU
Wanafunzi wote wa muda kamili wa Lowell High School wanaweza kuchukua masomo ya chuo kikuu cha mapema, lakini wanafunzi wa miaka ya mwanzo na ya mwisho watahitaji kutimiza masharti ya ustahiki wa programu, kujaza fomu zote zinazohitajika, na kupata idhini kutoka mzazi au mlezi kushiriki katika programu.
Masomo ya chuo kikuu cha mapema inayotolewa na ushiriki pamoja na Middlesex Community College ni bure kwa wanafunzi wa Lowell High School—gharama za masomo hulipiwa na ufadhili wa wilaya, programu za jimbo, msaada wa kibinafsi, na michango na punguzo kwa ada inayofanywa kikarimu na Middlesex Community College.
Katika hali nyingi, wanafunzi wa chuo kikuu cha mapema wataweza kupokea vifaa na vitabu vya masomo bila gharama kwao au kwa familia zao. Lakini, masomo kadhaa za chuo kikuu cha mapema zinazosomeshwa katika chuo kikuu cha Middlesex Community College ambazo ni wazi kwa wanafunzi wa miaka ya mwanzo na ya mwisho wa LHS, vinaweza kuhitaji wanafunzi kuazima au kununua vifaa kadhaa vya masomo. Iwapo wanafunzi au familia zao hawana uwezo, kwa sababu yeyote, kumudu vifaa hivyo vya masomo vinavyohitajika, wanapaswa kuwasiliana na timu yetu ya utegemezi ili kujadili chaguo. Lowell High School imejitolea kuondoa vizuizi vya kifedha kwa ushiriki wa chuo kikuu cha mapema, na mazungumzo yote na wafanyikazi wetu wa utegemezi ni siri.
Katika madarasa uya tisa na kumi, wanafunzi husajiliwa moja kwa moja kwa masomo ya alama moja ya chuo kikuu cha mapema kama sehemu ya Freshman Academy na Sophomore Academy.
Kwa madarasa ya kumi na moja na kumi na mbili, wanafunzi wanaweza kujisajili katika masomo ya chuo kikuu cha mapema walizochagua zinazotolewa na ushiriki pamoja na Middlesex Community College.
Orodha ya sasa ya masomo yote ya chuo kikuu cha mapema zinazotolewa kwa ushiriki na Middlesex Community College inaweza kupatikana HAPA. Somo za chuo kikuu cha mapema huweza kubadilika kulingana na kipindi au mwaka.
Masomo nyingi ya chuo kikuu cha mapema husomeshwa katika Lowell High School na walimu waliyothibitishwa wa shule ya upili. Lakini, wanafunzi wa miaka ya mwanzo na ya mwisho wataweza kujisajili katika masomo ya chuo kikuu cha mapema yaliyokubaliwa yanayosomeshwa na walimu wa chuo kikuu katika chuo kikuu cha Middlesex Community College.
Kwa wanafunzi wa miaka ya mwanzo na ya mwisho wanaotaka kuchukua masomo ya chuo kikuu cha mapema, masharti yafuatayo ya ustahiki yatahitaji kutimizwa: (1) matokeo ya PSAT au SAT ya alama 480 au zaidi katika kusoma na kuandika, (2) alama ya nokta ya wastani ya (GPA) 2.5 au juu zaidi, na (3) barua la kumpendekeza liloandikwa na mwalimu wa ELA wa mwanafunzi akiashiria kwamba mwanafunzi anamiliki ujuzi za kimsingi za kusoma na kuandika zinazohitajika kufanikiwa katika masomo ya kiwango cha chuo kikuu.
Wanafunzi wa miaka ya mwanzo na ya mwisho wanaweza kuchagua kuchukua masomo kadhaa ya chuo kikuu cha mapema kila kipindi cha masomo au mwaka wa shule. Wanafunzi wengi huchagua kwa kawaida kuchukua somo moja au mbili ya chuo kikuu cha mapema kila kipindi pamoja na masomo yao ya shule ya upili.
Wanafunzi wanaofanikiwa kukamilisha somo la chuo kikuu cha mapema hupata alama kutoka Lowell High School na Middlesex Community College. Alama za chuo kikuu cha mapema ni alama za kihakika za chuo kikuu na huweza kuhamishwa kwa vyuo vikuu kote marekani.
Wanafunzi wa Lowell High School wanaoshiriki katika chuo kikuu cha awali husajiliwa kirasmi kama wanafunzi wa muda nusu wa Middlesex Community College. Wanafunzi hawa hupokea kadi za kitambulisho za mwanafunzi wa Middlesex Community College, na wanastahiki kushiriki katika programu, vilabu, na sherehe zote za chuo kikuu—kama tu mwanafunzi mwingine wowote wa chuo kikuu.
Lowell High School imejitolea kutoa mwongozo, usaidizi, na utegemezi ambacho kila mwanafunzi anahitaji kushiriki kikamilifu na kwa mafanikio katika masomo ya chuo kikuu cha mapema. Timu ya utegemezi ya chuo kikuu cha awali cha Lowell High School inaweza kupatikana kutoa huduma za utegemezi pana kwa wanafunzi na familia zao.
MCHAKATO WA KUFANYA OMBI
Taarifa iliyo na maelezo zaidi kuhusu mchakato wa kufanya ombi la chuo kikuu cha mapema cha lowell linaweza kupatikana HAPA. Iwapo ungependa kuomba huduma za kiutafsiri au usaidizi wingine na mchakato wa kufanya ombi, tafadhali tumia taarifa ya mawasiliano hapa chini.
TAARIFA YA MAWASILIANO NA HUDUMA YA UKALIMANI
Ili kujifunza zaidi kuhusu masomo ya chuo kikuu cha mapema katika Lowell High School, tafadhali wasiliana na Timu ya Chuo Kikuu cha Awali ili kufanya ratiba ya ushauri. Iwapo utahitaji usaidizi wa ukalimani, tafadhali tuma baruapepe kwa earlycollege@lowell.k12.ma.us au wasiliana na Lowell Public Schools Family Resource Center (Kituo cha Rasilimali ya Taarifa ya Familia).